Sasa ni Papa Francis I !
13 Machi, 2013 - Saa 20:11 GMT
Papa Francis ahutubu mara ya kwanza
Kadinali Jorge Mario Bergoglio wa
Argentina amechaguliwa kuwa Papa mpya wa Kanisa Katoliwww.facebook.comki.
Kadinali Bergoglio anakuwa mtu wa kwanza kutoka Amerika
kusini kuchaguliwa kuwa Papa.
Mara tu baada ya kuchaguliwa alichagua jina la Papa Francis
I. Awali moshi mweupe ulishuhudiwa ukifuka kutoka bomba la
kutolea moshi katika kanisa la Sistine Chapel na kufuatiwa na kengele kupigwa.
Hii ilikuwa ni ishara kwa walimwengu kuwa makadinali ambao walianza mchakato wa
kumchagua Papa mpya hatimae walikuwa wamefaulu katika kazi yao.
Kadinali Bergoglio anachukuwa mahali pa Papa Benedict XVI,
ambaye alijiuzulu mwezi uliopita akisema hana nguvu na uwezo wa kuendelea
kuliongoza Kanisa Katoliki.
Makadinali 115 wamekuwa faraghani tangu siku ya Jumanne
alasiri na wakaanza mchakato wao kwa kupiga kura mara nne kwa siku.
Ilikuwa inahitajika kuwa angalau Makadinali 77 yaani
theluthi-mbili wangeliweza kumpigia kura mmoja wao ili aweze kutangazwa kuwa
Papa mpya.
Na kabla ya mchakato huo kuanza kulikuwa hakuna dalili za
kuonyesha nani angelichaguliwa.
Moshi mweupe
Maelfu ya watu kutoka sehemu mbali mbali duniani walikwa
wamekusanyika katika ukumbi wa Kanisa la St Peter tangu siku ya Jumanne.
Muda mfupi kabla ya Kadinali Bergoglio kujitokeza , maelfu
ya watu walionekana wakikimbia kuelekea ukumbi wa St Peters ili kuweza
kumshuhudia Papa mpya akitangazwa .
Papa Francis I
ni nani?
Alizaliwa Mjini Buenos Aires huko Argentina mwaka1936.
Papa Francis 1 ni mtu wa kwanza katika kipindi cha miaka
elfu moja (1,000) kwa mtu kutoka nje ya bara la Ulaya kutawazwa kuwa papa wa
Kanisa Katoliki.
Papa Francis 1 ni mwana wa Mtaliano aliyekuwa akifanya kazi
katika shirika la gari Moshi kabla ya kuhamia nchini Argentina miaka ya zamani.
Kama kadinali wa Jimbo la Buenos Aires ,Kadinali Bergoglio
amekuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya Argentina.
Hata hivyo Kadinali Bergoglio anapendwa sana na wafuasi wa
kanisa hilo huko Argentina na hasa watu maskini.
adinali Jorge Bergoglio, mwenye umri wa mwaka 76, kwa karibu
miaka yake yote kama Kasisi amehudumu nyumbani kwao Argentina.
Kadinali huyo wa Jimbo la Buenos Aires inasemekana aliibuka
nambari mbili wakati Papa Benedict alipochaguliwa mwaka 2005
Papa Francis akijitokeza
Anaaminika kuwa na ujuzi mkubwa ambao wengi wanasema
utamsaidia sana katika uongozi wake.
Katika maisha yake ya huduma kwa Kanisa Katoliki huko
Amerika Kusini ambapo Kanisa Katoliki lina waumini wengi zaidi duniani,
Kadinali Bergoglio ameibuka kuwa mtu anayependa sana udhabiti wa kisiasa katika
nchi zilizo katika bara la Amerika Kusini.
Bergoglio anasifiwa kwa kuleta mageuzi makubwa katika Kanisa
la Argentina huku katika eneo hilo la Amerika Kusini Kanisa bado linashikilia
itikadi za kale.
Good!
ReplyDelete