Monday, January 14, 2013

MAARIFA ILI KUONDOA MAZOEA

Matumizi ya neno "BAHATI"!

Mara nyingi katika mazungumzo yetu sisi wa swahili tume kuwa tukisema na kusikia wenzetu wakisema sentensi zifuatazo.
  •     Nilianguka bahati mbaya...........!
  •     Bahati mbaya sikumkuta..........!
  •     Mtoto ameumizwa kwa bahati mbaya.......!


Katika miundo hii ya sentensi ambayo inawakilisha miundo mingi ya zile sentensi tunazozizungumza tunatumia neneo BAHATI MBAYA  kimakosa. Japokuwa wataalamu wa lugha wanaeleza kuwa lugha huwa inatabia ya kuwa na kile kinachoweza kuitwa, "Mazoea yasiyokuwa na Mantiki" lakini sifa hii inapoendekezwa na kufanywa kuwa sababu au daraja la kupotosha matumizi ya maneno na miundo ya lugha, tunakuwa tunaharibu maana ya kuwa na kanuni mahususi za lugha. Vile vile tunakuwa tunaikosesha lugha haki yake ya kujidhibiti na kujibambulisha kama kitu pekee chenye uhai na sifa za pekee.

Hivyo basi, mimi napingana na matuizi yote ya neno BAHATI MBAYA kwani neno BAHATI mara zote na kwa asili yake linamaana chanya. Yaani huhusishwa na kitu jambo nzuri, hivyo ikishakuwa BAHATI hatuwezi kusema ni MBAYA tena. Kinyume chake ni neno MKOSI au BALAA. Kama mtu atatumia neno BAHATI MBAYA akimaanisha "hali ya kuto kukusudiwa", hali kadharika atakuwa anakosea. Mbadala wa neno hilo ni 'kuto kukusudiwa". 

Ninaandika makala hii nikitambua kuwa lugha na maneno katika lugha huweza kuwa na maana zaidi ya moja na kwamba lugha inatabia ya UWEKEVU. Katika hali kama hoyo mtu anaweza kuhoji kwa nini mtu ateseke kusema "KUTO KUKUSUDIWA" wakati lugha inawezwa kusinyaza miundo kwakutumia neno moja ili kuwasilisha mambo mengi? 

Sawa, hiyo ni sifa za lugha na zinapaswa kuzingatiwa, lakini kama nilivyosema mwamzo, kila kanuni inapotumiwa hata mazingiwa yasiyohusika inakuwa inaharibu mfumo na dhana nzima ya lugha kuwa ni kitu chenye kanuni zake ambazo zikikiukwa zinaondoa  uhalisia  na uasilia wa lugha husika.

AHSANTE KWA WASOMAJI
NINAKARIBISHA MAONI NA HOJA JUU YA MADA HII.
Okoa Simile!